bunge wa Jimbo la Nanyamba Mhe Chikota leo tarehe 31/12/2024 amekabidhi Mashine 10 za kubangua korosho kwa vikundi vya wajasiriamali na Mjasiriamali mmoja mmoja wa Halmashauri ya Mji Nanyamba.
Mhe Chikota amesema kuwa mashine hizo zitasaidia kuongeza thamani ya zao la korosho pia zitasaidia vikundi hivyo vya wajasiriamali hao kujiongezea kipato chao cha kila siku huku akiwahasa vikundi hivyo kuepukana na tabia baadhi ya wana kikundi kujimilikisha mashine hizo.Vikundi vilivyonufaika na mashine hizo ni kikundi cha hamasa kutoka Mtaa wa Nanyamba B kata ya Nanyamba kimepata mashine 4, kikundi cha Upendo kutoka Kijiji cha Nitekela kimepata mashine 4, Mjasiriamali Zuhura Ismail Mmadi amepata mashine moja na Mjasiriamali Aziza Ally amepata mashine moja.Ndugu Kaisi Abdala Lukanga akizungumza kwa niaba ya wana kikundi hao amemshukuru Mhe Chikota kwa kuwapatia mashine hizo kwani zitasaidia kuongeza kipato chao cha kila siku nae Bi Zuhura Ismail Mmadi akiwakilisha wajasiriamali amemshukuru Mhe Chikota kwa kuwapatia Mashine hizo pia.
NANYAMBA, MTWARA.
Sanduku la Barua: P.O.BOX 1490,
Simu: +255
Simu:
Barua pepe: td@nanyambatc.go.tz
Copyright ©2016 Nanyambatc . All rights reserved.