Mbunge wa Jimbo la Nanyamba kuhakikisha Jimbo la Mji huo unakuwa wa kisasa leo tarehe 2/2/2025 amezindua mradi wa ufungaji wa Taa za barabarani Katika Halmashauri ya Mji Nanyamba, katika uzinduzi huo wa Taa 132 zenye thamani ya shilingi million mia nne hamsini na tisa elfu (459,000,000) zaidi ya Barabara tano zitaunganishwa na Taa hizo.
Akisoma taarifa kwa mbunge Afisa Mipango wa Mji Nanyamba Ndg Walyama Sospeter Tundosa alizitaja barabara zilizopitiwa na mradi huo ni Barabara ya Chikota, barabara ya Msijute, barabara ya Kinondoni, barabara ya Kitaya na barabara ya Hawa Ghasia.
Mhe Chikota amewaomba Wananchi wa Halmashauri hiyo kutunza miradi hiyo inayotekelezwa na Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania ili lengo la Wananchi haoǰ liweze kutimia, aliongeza kwa kusema kuwa mradi huo utasaidia pia kuongezeka kwa kipato kutokana hata muda wa usiku kuweza kufanya biashara kando kando ya barabara hizo alimalizia kwa kusema maneno hayo.
Mradi huo upo chini ya mkandarasi Afro Solar Germany Co. Limited katika mradi huo wa Taa gharama zake zipo chini ya mradi wa usambazaji wa umeme vijijini (REA) kwa kusaidiniana na Halmashauri ya Mji Nanyamba kwa asilimia 50 kwa 50 kupitia mapato yake ya Ndan
NANYAMBA, MTWARA.
Sanduku la Barua: P.O.BOX 1490,
Simu: +255
Simu:
Barua pepe: td@nanyambatc.go.tz
Copyright ©2016 Nanyambatc . All rights reserved.