Katika kuhakikisha miradi yote inayoendelea kutekelezwa Mji Nanyamba inakamilika kabla ya Disemba 30, 2024 Mkurugenzi wa Mji Nanyamba Mhandisi Mshamu Munde leo ameendelea kutembelea miradi mbalimbali katika kata ya Nyundo na Hinju.
Katika ziara hiyo akiambatana na baadhi ya Wakuu wa Divisheni na Vitengo ametembelea shule mpya ya mkondo mmoja katika shule ya Msingi Nyundo B, Kituo cha afya Nyundo pamoja na ujenzi wa shule mpya ya sekondari kata ya Hinju.
Ziara hiyo ya Mkurugenzi Munde amewasisitiza wasimamizi wa miradi hiyo kuwa eneo la mradi ili kuendelea kuwahimiza mafundi waweze kujenga kwa ubora unaotakiwa na kufuata mkataba unataka nini kipindi chote cha ujenzi wa miradi hiyo
NANYAMBA, MTWARA.
Sanduku la Barua: P.O.BOX 1490,
Simu: +255
Simu:
Barua pepe: td@nanyambatc.go.tz
Copyright ©2016 Nanyambatc . All rights reserved.