HAKIKISHENI MIRADI INAKUWA YENYE UBORA NA KIWANGO MKURUGENZI MUNDE AWAHIMIZA MAFUNDI.
Ikiwani siku ya pili ya ziara ya Mkurugenzi wa Mji Nanyamba Mhandisi Mshamu Munde leo tarehe 17/11/2024 ya kutembelea na kuona miradi inayoendelea kutekelezwa katika sekta za afya na elimu kwa lengo la kusikiliza na kutatua changamoto mbalimbali zilizopo katika miradi na kuweza kutatua mapema.
Mhandisi Munde amewaeleza mafundi hao ya kuwa watumie nafasi waliyopata kama wanajenga nyumba zao kwa kuzingatia ubora wa ujenzi na usafi unaotakiwa hususani hatua ya umaliziaji amesema ndiko kwenye changamoto kubwa na katoa rai kwa mafundi hao kuwa hatasita kumuondoa fundi kama hafuati hatua za ujenzi bora unaotakiwa na serikali.
Katika ziara hiyo Mhandisi Mshamu ametembelea shule ya msingi Mwenge yenye mradi wa madarasa Matundu ya vyoo na nyumba ya Mwalimu moja kwa mbili, ametembelea shule ya Msingi Mnongodi ambapo kuna mradi wa vyumba vya Madarasa na matundu ya Vyoo, shule ya msingi Likwaya katika mradi wa Vyumba vya madarasa na matundu ya vyoo, shule ya Msingi, Nitekela ambako kuna ukarabati wa vyumba vya madarasavna ujenzi wa matundu vyoo, Kituo cha Afya Nyundo, ujenzi wa shule mpya ya mkondo mmoja Shule ya Msingi Nyundo B, shule mpya ya sekondari Hinju kupitia mradi wa uboreshaji wa elimu Sekondari (SEQUIP), na mradi wa mwisho ni wa nyumba ya Mwalimu moja kwa mbili na ujenzi wa shule ya kidato cha tano Mtiniko sekondari.
NANYAMBA, MTWARA.
Sanduku la Barua: P.O.BOX 1490,
Simu: +255
Simu:
Barua pepe: td@nanyambatc.go.tz
Copyright ©2016 Nanyambatc . All rights reserved.