Msimamizi wa Uchaguzi Halmashauri ya Mji Nanyamba Mhandisi Mshamu Ali Munde leo tarehe 23/11/2024 amefungua Semina kwa wasimamizi wa vituo vya kupigia kura, Msimamizi huyo amewaeleza kuwa wakafanye kazi waliotumwa na serikali.
Zaidi ya wasimamizi 600 wamepatiwa semina hiyo ambapo wanatarajia kufanya kazi siku ya Uchaguzi tarehe 27 Novemba 2024 siku ya jumatano. Mhandisi Munde amewataka kufuata kanuni za Uchaguzi wa Serikali za mitaa inavyotekelezwa.
Katika semina wasimamizi hao pia wamekula viapo vya utii kwa kufanya kazi hiyo bila kujitokeza changamoto yoyote ili Uchaguzi huo unafanyika kwa amani na utulivu.
NANYAMBA, MTWARA.
Sanduku la Barua: P.O.BOX 1490,
Simu: +255
Simu:
Barua pepe: td@nanyambatc.go.tz
Copyright ©2016 Nanyambatc . All rights reserved.