MTUWASA WASAINI MKATABA BILIONI 5.6 ZA MRADI WA MAJI WA MNYAWI KATIKA HALMASHAURI YA MJI NANYAMBA.
Tukio hilo la utiaji Saini wa mkataba wa ujenzi wa mradi wa Maji Halmashauri ya Mji Nanyamba limefanyika Julai 06.07.2023 kwenye Ofisi ya Mkuu Wa Wilaya ya Mtwara Mhe. Hanafi Msabaha.
Mradi huo uliopo Kijiji cha Mnyawi Kata ya Milangominne, ambao umegharimu kiasi cha Shilingi Bilioni Tano na Milioni Mia Sita (5.6). Mradi Huo utakuwa ni wakufumua Miundombinu Yote ya zamani na kutandaza upya mabomba, Ujenzi wa Tenki la Lita Milioni Moja na kuongeza idadi ya visima kwenye chanzo ili kuondoa changamoto ya upatikanaji wa Maji katika Halmashauri ya Mji Nanyamba na Vijiji vyake vyote.
Akiongea Mbunge wa Jimbo la Nanyamba Mhe. Abdallah Dadi Chikota Mara baada ya kushuhudia Utiaji wa Saini wa Mkataba ameishukuru Serikali ya Awamu ya sita chini ya Mhe. Dkt Samia Suluhu Hassan kwa kutoa Fedha hizo ili kuibadilisha miundombinu ambayo ilikuwa chakavu na kuongeza tanki lenye ujazo mkubwa.
NANYAMBA, MTWARA.
Sanduku la Barua: P.O.BOX 1490,
Simu: +255
Simu:
Barua pepe: td@nanyambatc.go.tz
Copyright ©2016 Nanyambatc . All rights reserved.