Mkuu wa Mkoa wa leo tarehe 24/1/2025 amezindua kampeni ya kitaifa ya Msaada wa kisheria ya Mama Samia Legal Aid katika viwanja vya mashujaa, katika uzinduzi huo amezitaka kamati zote zilizoteuliwa katika Halmashauri zao kwenda kuwasaidia wananchi wao kupata elimu hiyo ya kisheria.
Mkuu wa Mkoa wa Mtwara Mhe Kanali Patrick Kenan Sawala amewahasa wananchi pia kutumia fursa hiyo kwenda kutatua changamoto zao kupitia kampeni hiyo ya msaada wa kisheria.Rc Sawala amesema kuwa kampeni hiyo itadumu kwa siku 10 kuanzia leo tarehe 24/1/2025 hadi tarehe 2/2/2025 kwa Halmashauri tisa zote za Mkoa wa Mtwara, kampeni ya Msaada wa kisheria itadumu kipindi cha muda wa miaka mitatu 2023 hadi 2026.Alihitimisha kwa kusema lengo la kampeni hii ina lengo la kutoa elimu ya msaada wa kisheria kwa wananchi hususani masuala ya ukatili wa kijinsia, migogoro ya Ardhi, Mirathi na masuala yahusuyo haki za kibinadamu.
NANYAMBA, MTWARA.
Sanduku la Barua: P.O.BOX 1490,
Simu: +255
Simu:
Barua pepe: td@nanyambatc.go.tz
Copyright ©2016 Nanyambatc . All rights reserved.