Leo tarehe 13/9/2024 Shirika lisilo la Kiserikali la Sports Development Aid (SDA) kwa kushirikiana na wanakikundi wa uhamasishaji Jamii katika Halmashauri ya Mji Nanyamba limeweza kutoa Elimu ya kupambana na Ukatili kwa jamii kata ya Mtimbwilimbwi.
Katika juhudi hizo waliandaa mafunzo ya kuelimisha jamii kuhusu athari za ukatili na kumsimamia mtoto wa kike atimize ndoto zake.
Kupitia michezo mbalimbali na mafunzo yaliyoandaliwa na wadau kama vile maigizo mafupi ya jukwaani (Forum Theatre), Mpira wa miguu, kukimbiza kuku na ngoma zilifanyika zenye ujumbe wa kuhamasisha jamii juu ya kupinga ukatili kwa Watoto na Wanawake unaofanywa na baadhi ya watu ndani ya jamii na kuhimiza mshikamano katika jamii huku zawadi mbalimbali zikitolewa kwa washindi wa tamasha hilo.
NANYAMBA, MTWARA.
Sanduku la Barua: P.O.BOX 1490,
Simu: +255
Simu:
Barua pepe: td@nanyambatc.go.tz
Copyright ©2016 Nanyambatc . All rights reserved.