Halmashauri ya Mji Nanyamba leo tarehe 13/02/2024 imefanya mafunzo kwa wadau wa afya na maendeleo ili kuhamasisha kampeni ya kitaifa ya utoaji chanjo za surua na rubella kwa watoto wote walio katika umri wa miezi 9 mpaka chini ya miaka 5. Zoezi hilo la chanjo linaratibiwa na wizara ya afya litaanza tarehe 15-18 Februari 2024.
Surua na Rubella ni magonjwa yanayosabishwa na virusi na kuenezwa kwa njia ya hewa na husababisha madhara kwa afya na vifo kwa watoto walio na umri chini ya miaka mitano.
Akielezea dalili za magonjwa hayo, mtaalamu wa chanjo Bw. Liputi alisema “Dalili za ugonjwa wa surua ni pamoja na Homa, mafua, kikohozi, macho kubwa mekundu na kutoa majimaji; vipele vidogo vidogo ambavyo huanza kwenye paji la uso, nyuma ya masikio na kusambaa usoni mwili mzima. Rubella dalili zake hufanana na ugonjwa wa surua.”
Lengo na Halmashauri ya Mji Nanyamba ni kutoa chanjo kwa watoto 14,783 ambayo itapatikana katika vituo vya kudumu vya afya pamoja na vituo vya muda vitakavyoundwa
NANYAMBA, MTWARA.
Sanduku la Barua: P.O.BOX 1490,
Simu: +255
Simu:
Barua pepe: td@nanyambatc.go.tz
Copyright ©2016 Nanyambatc . All rights reserved.