Leo tarehe 09/02/2024 ikiwa ni siku ya pili ya baraza la madiwani kupokea na kujadili taarifa za kamati kiutendaji Kwa robo ya pili ya mwaka 2023/24; Kaimu Mkurugenzi wa Halmashauri ya Mji Nanyamba, Wakili Prosper Kisinini awasilisha taarifa za nafasi ya Halmashauri ya Mji Nanyamba kwenye Mwenge Uhuru, matokeo ya mtihani wa darasa la saba na kidato cha nne.
“Taarifa ya kwanza ni matokeo ya Mwenge wa Uhuru, Halmashauri yetu ya Mji Nanyamba imeshika nafasi ya pili kati ya halmashauri 9. Taarifa ya pili ni matokeo ya mtihani wa darasa la saba, halmashauri ya Mji Nanyamba imeshika nafasi ya pili kimkoa. Na taarifa ya tatu ni matokeo ya kidato cha nne, kimkoa halmashauri ya Mji Nanyamba imeshika nafasi ya kwanza.” Alieleza kaimu Mkurugenzi.
NANYAMBA, MTWARA.
Sanduku la Barua: P.O.BOX 1490,
Simu: +255
Simu:
Barua pepe: td@nanyambatc.go.tz
Copyright ©2016 Nanyambatc . All rights reserved.