TIMU YA LISHE MJI NANYAMBA YAENDELEA KUELIMISHA JAMII KUHUSU LISHE YA MAMA NA MTOTO
Timu ya lishe Mji Nanyamba ikiongozwa na Afisa Lishe Bi Pilly Mpelengani imefika kata yavChawi na Chawi kwa lengo la kuendelea na kampeni ya kuimarisha afya ya mama na mtoto.
Mama wajawazito wamepatiwa vipimo vya afya, elimu ya lishe bora na darasa la mapishi ya vyakula vya kuongeza damu.
“Mama mwenye lishe bora ni mtoto mwenye afya bora,” amesema Afisa Lishe Bi Pilly Mpelengani.
Kampeni hii imeendelea kugusa maisha ya kina mama na familia zao kwa kutoa maarifa ya afya bora kila siku.
Timu ya lishe imeendela kusisitiza umuhimu wa huduma za kina na ufuatiliaji wa afya kwa mama wajawazito ili kugundua mapema changamoto kama upungufu wa damu na kuzuia madhara yanayoweza kuepukika
NANYAMBA, MTWARA.
Sanduku la Barua: P.O.BOX 1490,
Simu: +255
Simu:
Barua pepe: td@nanyambatc.go.tz
Copyright ©2016 Nanyambatc . All rights reserved.