TIMU YA LISHE MJI NANYAMBA YAENDELEA KUTOA ELIMU YA MAMA NA MTOTO.
Leo tarehe 21 Julai 2025 Timu ya lishe kwa kushirikiana na wahudumu wa afya ya jamii imetembelea Kijiji cha Mpanyani kata ya Kiyanga katika kuendeleza kampeni ya kuimarisha afya ya mama na mtoto.
Katika zoezi hilo Mama wajawazito wamepatiwa huduma za uchunguzi wa hali upimaji wa wingi wa damu na Malaria pamoja na elimu ya lishe bora ili kupunguza changamoto za kiafya wakati wa ujauzito.
Mbali na vipimo, darasa la mapishi limefanyika likiwaelimisha kina mama kuhusu aina ya vyakula vinavyoongeza damu na virutubisho vinavyohitajika katika kipindi cha ujauzito ikiwa lengo kuu ni kuhakikisha mama anapata lishe yenye uwiano bora na hatimaye kujifungua mtoto mwenye afya bora.
Timu ya lishe imeendelea kusisitiza kuwa afya ya mama ni msingi wa familia yenye nguvu, na kila mama mjamzito anastahili huduma za kinga na ufuatiliaji wa afya kwa wakati. Zoezi hili pia limetoa nafasi kwa watoa huduma kugundua mapema changamoto kama upungufu wa damu na kuunganisha huduma za matibabu kwa waliosaidiwa.
Pongezi ziende kwa viongozi wa kijiji na wahudumu wa afya walioungana nasi kufanikisha huduma hizi, kampeni kama hizi ni sehemu ya jitihada za kuhakikisha hakuna mama anayepoteza maisha kwa sababu ya changamoto za ujauzito ambazo zinaweza kuzuilika.
NANYAMBA, MTWARA.
Sanduku la Barua: P.O.BOX 1490,
Simu: +255
Simu:
Barua pepe: td@nanyambatc.go.tz
Copyright ©2016 Nanyambatc . All rights reserved.