Timu ya kampeni ya msaada wa kisheria ya @mslegalaidcampaign kutoka wizara ya katiba na sheria tarehe 27/1/2025 imekutana na timu ya Menejimenti na watendaji wa kata kuwapa mafunzo yatakayowawezesha kufanya kazi kwa kuzingatia haki za binadamu na utawala bora katika maeneo yao ya kazi mafunzo hayo yamefanyika katika ukumbi mdogo wa Mji Nanyamba.Mafunzo hayo yatafungua ufahamu wetu wa namna bora ya kushauri na kuongoza watu wetu, ofisi zetu zinatakiwa kuwa msaada na kimbilio kwa wananchi.
Tujiulize tunafanyaje kazi na viongozi wenzetu bila kuingiliana kimajukumu tunapaswa tushirikiane ili wananchi wapate huduma iliyo bora bila manung'uniko.
Wakili Prosper Kisinini kutoka wizara ya @katibanasheria_ aliwaeleza misingi ya utawala bora kuwa ni pamoja na uwazi, uwajibikaji, utawala bora, utawala wa sheria, usawa, uadilifu, ufanisi wenye tija, maridhiano, ushirikishaji na mwitikio kwa kushirikiana katika nyanja zote zinazogusa utawala bora.
NANYAMBA, MTWARA.
Sanduku la Barua: P.O.BOX 1490,
Simu: +255
Simu:
Barua pepe: td@nanyambatc.go.tz
Copyright ©2016 Nanyambatc . All rights reserved.