Halmashauri ya Mji Nanyamba tarehe 6/2/2025 imeketi kikao chake Cha robo ya pili mwaka wa fedha 2024/2025 kujadili taarifa za kata na kamati mbalimbali za Halmashauri.
Mkuu wa Wilaya ya Mtwara Mhe Abdallah Mwaipaya akizungumza mbele ya Baraza la waheshimiwa Madiwani amesema kuwa Kuna timu kutoka wizara ya kilimo zipo kwenye kata za Mji Nanyamba kutokana na changamoto ya wakulima kutolipwa fedha zao kwa wakati na mkanganyiko uliopo wa kulipwa wakulima bei tofauti timu hiyo iachwe iweze kufanya kazi yao iliyowaleta Nanyamba.
Pia Dc Mwaipaya aliendelea kusisitiza suala zima la usimamizi wa makusanyo ya mapato na kusimamia wanafunzi wote waripoti kwa wakati hadi kufika Februari asilimia 83 wawe wamesharipoti shuleni.
Katika Kikao hicho Cha Baraza la waheshimiwa Madiwani ilihudhuliwa Mkuu wa Wilaya ya Mtwara, Kamati ya Ulinzi, viongozi wa vyama vya Siasa, wakuu wa Taasisi mbalimbali, Wakuu wa Divisheni na Vitengo pamoja na watendaji wa Kata za Mji huo.
NANYAMBA, MTWARA.
Sanduku la Barua: P.O.BOX 1490,
Simu: +255
Simu:
Barua pepe: td@nanyambatc.go.tz
Copyright ©2016 Nanyambatc . All rights reserved.