Bodi ya korosho Tanzania leo tarehe 05/01/2024 imefika Halmashauri ya Mji Nanyamba kuzungumza na waheshimiwa madiwani kuhusu mradi wa kongani la viwanda vya korosholililopo kijiji cha Maranje, kata ya Mtiniko unaotarajia kuongeza ubanguaji korosho nchini pamoja na kuzalisha bidhaa zingine zitokanazo na korosho kama vile mafuta ya ganda la korosho na mazao mengine ikiwemo ufuta.
Mkurugenzi wa bodi ya korosho ameeleza faida zitakazopatikana kutokana mradi huo ni pamoja na uhakika wa soko la korosho ghafi pamoja na korosho karanga.
“Mradi pia utaleta fursa za ajira zaidi ya 35,000 kwa wananchi wote hasa wanaozunguka eneo la mradi; pia Halmashauri itaongeza mapato kutokana na tozo mbalimbali na serikali itapata zaidi ya dola milioni 300 kwa miaka 10 toka kusimikwa kwa mradi.” Alieleza mkurugenzi wa bodi ya korosho.
Halmashauri ya Mji Nanyamba imetenga Ekari 1,571.78 kwaajili ya utekelezaji wa mradi huo ambapo ujenzi utahusisha: Viwanda 10 vya kubangua korosho ghafi jumla ya tani 300,000 kwa mwaka ambapo kila kimoja kitakuwa na uwezo wa kubangua tani
30,000 kwa mwaka; Viwanda vitatu vya kuchakata ufuta tani 300,000 kwa mwaka; Viwanda viwili wa kukamua mafuta ya ganda la korosho (CNSL) vyenye uwezo wa kuchakata maganda vote yatakayo zalishwa katika kongani hilo; Viwanda vya kuchakata korosho karanga zote zitakazobanguliwa katika kongani hilo; Viwanda vya kuchakata mabibo.
Pia mradi utahusisha ujenzi wa Maabara kwa ajili ya ufuta na korosho karanga; Maghala nane ambayo kila moja litakuwa na ukubwa wa mita za mraba 25,000; Jengo la utawala lenye gorofa tatu; Maeneo wazi manne ya kukaushia korosho ghafi tani 30,000; Karakana(garage) kwa ajili ya matengenezo ya mitambo na magari ya kongani; Kantini ya chakula; Zahanati kwa ajili ya kuhudumia wafanyakazi na wananchi wanaozunguka eneo la mradi.
NANYAMBA, MTWARA.
Sanduku la Barua: P.O.BOX 1490,
Simu: +255
Simu:
Barua pepe: td@nanyambatc.go.tz
Copyright ©2016 Nanyambatc . All rights reserved.