Mkurugenzi wa Halmashauri ya Mji Nanyamba Bi Zainab Mgomi, Leo tarehe 23 julai 2025 ameendelea na zoezi la utambulishaji miradi ya maendeleo mpango wa BOOST kwa siku ya pili.Miradi imetambulishwa katika vijiji vya Hinju, Njengwa, Nyundo II na Niyumba.
Akizungumza katika zoezi la utambulisho miradi ya maendeleo iliyotambulishwa ni
i/ Ujenzi wa majengo ya shule Mkondo Mmoja katika shule ya msingi Njengwa (chakavu), mradi ambao umetengewa pesa kiasi Cha Tsh milioni 314
ii/ Ujenzi wa madarasa 2 na matundu 6 ya vyoo E/Awali katika Kijiji Cha kitachi mradi uliotengewa Tsh 67,300,000
iii/ Ujenzi wa madarasa 2 matundu 6 ya vyoo E/Awali na matundu 6 ya vyoo E/Msingi na ukarabati wa shule Kijiji Cha Nyundo II mradi uliotengewa 127,500,000
iv/ Ujenzi wa madarasa 2 matundu 6 ya vyoo E/Awali na matundu 4 ya vyoo E/Msingi na ukarabati wa shule katika Kijiji Cha Niyumba mradi uliotengewa 124,000,000
Mkurugenzi wa Mji amemshukuru Mh Rais Dkt Samia Suluhu Hassan kwa kuleta pesa za miradi ya maendeleo ikiwa ni utekelezaji wa ilani ya Chama Cha Mapinduzi (CCM)
Ametoa wito kwa wananchi wa vijiji vyote kuipokea miradi kwa mikono miwili huku akiwasihi kushiriki kwenye kazi za awali kama vile kusafisha eneo la mradi, uchimbaji wa msingi na ujazaji kifusi ikiwa ni sehemu ya mchango wa nguvu ya jamii katika miradi ya maendeleo.
Aidha aliwakumbusha walimu viongozi na timu za vijiji kutumia mfumo wa manunuzi NeST wakati wa utekelezaji wa miradi lakini pia kuweka kumbukumbu ya matumizi yote ya pesa za miradi na nyaraka zote za malipo kuhifadhiwa kwa usahihi.
NANYAMBA, MTWARA.
Sanduku la Barua: P.O.BOX 1490,
Simu: +255
Simu:
Barua pepe: td@nanyambatc.go.tz
Copyright ©2016 Nanyambatc . All rights reserved.