Mashirika yasiyo ya kiserikali ya Tanzania Life Improvement Association (TALIA), Bakwata Aid (BAKAID) na Faidika Wote Pamoja (FAWOPA) kwa kushirikiana na Ofisi ya Maendeleo ya Jamii Halmashauri ya Mji Nanyamba wazindua siku 16 za kupinga ukatili wa Kijinsia kijinsia leo tarehe 29/11/2024 katika kata kata ya Namtumbuka.
Katika uzinduzi huo wa siku 16 za kupinga ukatili uliambatana na utoaji wa msaada wa kisheria kwa wananchi wa kata ya Namtumbuka, utoaji wa elimu, huduma za kiafya Pamoja na utoaji wa elimu kuhusu ndoa za utotoni ambapo mdahalo ulifanyika kubaini sababu za ndoa za utotoni.
Mdahalo huo ulizingatia hasa nafasi ya Wazazi katika kupunguza ndoa za Utotoni, nafasi za vijana katika kupunguza ndoa za utotoni Pamoja na nini kifanyike ili kuweza kupunguza ndoa za utotoni ambapo wananchi mbalimbali walijitokeza na kuchagia mada.
NANYAMBA, MTWARA.
Sanduku la Barua: P.O.BOX 1490,
Simu: +255
Simu:
Barua pepe: td@nanyambatc.go.tz
Copyright ©2016 Nanyambatc . All rights reserved.