Halmashauri ya Mji Nanyamba kuhakikisha viongozi wote waliochaguliwa katika uchaguzi wa Serikali za Mitaa uliofanyika tarehe 27 Novemba 2024 mapema leo tarehe 18/12/2024 wameanza kupatiwa mafunzo ya Uongozi yatakayodumu kwa siku mbili tarehe 18-19/12/2024.Kaimu Mkurugenzi Ndg Walyama Sospeter Tundosa amewahasa viongozi hao kwenda kuwatumikia wananchi kwa kutoa huduma inayotakiwa na serikali bila kubaguana, vilevile amewataka kusimamia miradi inayoletwa katika maeneo yao kwa kushirikiana na serikali ya awamu ya sita chini ya Rais Dkt Mheshimiwa Samia Suluhu Hassan kwa kuwahimiza wananchi umuhimu wa kujitolea katika miradi hiyo inayotekelezwa.
Pia Kaimu Mkurugenzi Ndg Walyama Tundosa aliendelea kuwasisitiza kwenda kufanya kazi bega kwa bega na watendaji wao katika kuhakikisha usimamizi wa ukusanyaji wa mapato unasimamiwa ipasavyo ili fedha hizo ziweze kusaidia kutatua changamoto mbalimbali ikiwa ujenzi wa miradi ya maendeleo katika maeneo yao.
NANYAMBA, MTWARA.
Sanduku la Barua: P.O.BOX 1490,
Simu: +255
Simu:
Barua pepe: td@nanyambatc.go.tz
Copyright ©2016 Nanyambatc . All rights reserved.