Serikali imeagiza kuanza kutolewa kwa huduma za afya katika kituo cha afya majengo, dinyecha na kiromba wilayani Nanyamba mkoani Mtwara ndani ya miezi mitatu kwa kuwa ujenzi wa majengo yake yote yapo katika hatua za mwisho.
Akitoa maagizo ya Serikali, Naibu Katibu Mkuu Ofisi ya Rais TAMISEMI, Dkt. Zainab Chaula amesema hakuna haja ya kuchelewesha kutoa huduma za afya katika kituo cha afya majengo, dinyecha na kiromba kwa kuwa wananchi wanahangaika kuitafuta huduma hiyo mbali wakati miundombinu ya kituo hicho ipo katika hatua za mwisho.
“kwa sababu watu wanahitaji huduma, wanafanya mawasiliano sehemu nyingine ili kupata huduma ambayo hapa haipo, lakini ndani ya miezi mitatu lazima huduma zianze kutolewa, Mganga Mkuu wa Wilaya Nanyamba andaa andiko ili mchakato wa kuanzisha kituo uanze mara moja”
Dkt. Chaula ametoa agizo hilo mbele ya Mkurugenzi wa Halmashauri ya wilaya Nanyamba, Mganga Mkuu wa Mkoa Mtwara, wataalam wengine kutoka Ofisi ya Mkuu wa Mkoa na Ofisi ya Rais TAMISEMI wakati akiongea na wananchi katika mkutano ulioandaliwa baada ya kukagua miundombinu ya kituo cha afya majengo.
Aidha, Chaula amesema wakati Serikali inawapangia vituo watumishi wapya 6,180 imewaweka katika mpango wa kuwapangia vituo watumishi wapya katika vituo vipya vinavyokamilika kwa wakati, lakini pia ametoa angalizo kwa wananchi, watumishi na viongozi wote wilayani Nanyamba kuweka mazingira rafiki ili watumishi wapya wasipatwe na hali ya kuyakataa mazingira ya kazi bali watoe motisha kutatua changamoto hiyo.
Hassan Mnengu ni mwananchi wa kijiji cha majengo anasema huenda usumbufu waliokuwa wakiupata utakwisha kwa kufuata huduma za afya mbali na kijiji chao kwa hivi sasa.
NANYAMBA, MTWARA.
Sanduku la Barua: P.O.BOX 1490,
Simu: +255
Simu:
Barua pepe: td@nanyambatc.go.tz
Copyright ©2016 Nanyambatc . All rights reserved.