Waheshimiwa Madiwani, viongozi wa chama Mtwara vijijini, baadhi ya wakuu wa Divisheni na Vitengo waendelea na ziara ya kutembelea na kujionea kiwanda cha Matofali kinachomilikiwa na Jiji la Mwanza.
Ziara hiyo ya waheshimiwa madiwani kwa upande wa kiwanda cha matofali imetokana na kufanya vizuri kiwanda chao cha Jiji la Mwanza na Halmashauri ya Mji Nanyamba pia kuwa na kiwanda cha usambazi wa madini ya ujenzi pamoja na matofali ili wakirudi Nanyamba waweze kukisimamia vizuri kiwanda hicho.
Waheshimiwa hao waliwapongeza Jiji la Mwanza kuwa na mtambo mkubwa wa ufyatuaji tofali nne kwa pamoja ambayo kwa siku inatumia mifuko sitini Waheshimiwa hao wamehaidi kulifanyia kazi kwa kukiongezea uwezo wa mitambo kiwanda cha Nanyamba cha ufyatuaji wa tofali.
Kwa upande wa Mkurugenzi wa Mji Nanyamba Mhandisi Mshamu Munde amewahakikishia waheshimiwa yale yote waliyojifunza yupo tayari kuyafanyia kazi kwa maelekezo yao ili mradi huo uwe wenye tija na kunufaisha Halmashauri nzima ya Nanyamba si kwa miradi ya serikali tuu hata wananchi watakaohitaji huduma hiyo.
NANYAMBA, MTWARA.
Sanduku la Barua: P.O.BOX 1490,
Simu: +255
Simu:
Barua pepe: td@nanyambatc.go.tz
Copyright ©2016 Nanyambatc . All rights reserved.