Waheshimiwa Madiwani, Wakuu wa Divisheni na Vitengo pamoja na viongozi wa Chama cha Mapinduzi Mtwara vijijini wahitimisha ziara Jijini Mwanza kwa kutembelea Kisiwa cha Saanane kikichopo Wilaya ya Nyamagana.
Viongozi hao wa chama na Halmashauri ya Mji Nanyamba katika kuhakikisha kuunga juhudi za utalii wa ndani kwa kutembelea kisiwa hicho cha @saananeisland_nationalpark wamejionea wanyama mbalimbali kama vile Simba, Swala, Nyumbu na ndege aina ya Tausi.
Wakizungmza baada ya ziara hiyo wamewashukuru Halmashauri ya Jiji la Mwanza kwa mapokezi mazuri na kuwapa ushirikiano kila walipokuwa wanahitaji ufafanuzi walipewa ushirikiano wa kutosha.
Walimalizia kwa kusema yote waliyojifunza kwenye dampo la taka ngumu, kiwanda cha tofali, stand na mbinu za ukusanyaji wa mapato wanaenda kuyafanyia kaziì kwasababu ziara hiyo imekuwa yenye tija zaidi.
NANYAMBA, MTWARA.
Sanduku la Barua: P.O.BOX 1490,
Simu: +255
Simu:
Barua pepe: td@nanyambatc.go.tz
Copyright ©2016 Nanyambatc . All rights reserved.