Wanafunzi wa Shule ya Sekondari Mnima kata ya Mnima wapatiwa mafunzo ya msaada wa kisheria ya @mslegalaidcampaign yanayoratibiwa na Wizara ya @katibanasheria, Mratibu wa Mama Samia Legal Aid kwa Halmashauri ya Mji ndg @kabado awaeleza wanafunzi hao kutosita kuibua vitendo vya ukatili wanavyofanyia kwa kunyimwa haki zao za msingi.
Ikiwa leo tarehe 28/1/2025 siku ya nne toka kampeni hiyo izinduliwe, kwa upande wa Afisa Ustawi wa Jamii Mji Nanyamba Ndg Joseph Mwasikanda wanafunzi hao aliwatahadharisha juu ya kutojihusisha na makundi ya kihuni kwani wakifanya hivyo itapelekea kushindwa kufanya vizuri katika masomo yao na ndoto zao walizojiwekea kutotimia.
NANYAMBA, MTWARA.
Sanduku la Barua: P.O.BOX 1490,
Simu: +255
Simu:
Barua pepe: td@nanyambatc.go.tz
Copyright ©2016 Nanyambatc . All rights reserved.