Na Afisa habari.
Wananchi wa kijiji cha Majengo kata ya Njengwa, Halmashauri ya mji Nanyamba wamemfurahisha Mkuu wa Mkoa wa Mtwara Mhe. Gelasuis Gaspar Byakanwa kwa namna ambayo wamekuwa wakishiriki katika ujenzi wa kituo cha Afya cha Majengo.
Akihutubia wananchi wa kijiji cha majengo, Mkuu wa Mkoa amewasifu na kuwapongeza wananchi hao kwa juhudi wanazozifanya kushirikiana na serikali ya awamu ya tano katika shughuli za maendeleo. Pamoja na hayo, Mkuu wa Mkoa ametoa mifuko 200 ya saruji kwa ajili ya ujenzi wa wodi ya wanaume katika kituo cha afya hicho.
“Nimevutiwa na kufurahishwa na namna wananchi wa kijiji cha Majengo mnavyojitolea katika shughuli za maendeleo. Nimesikia mnaomba muongezewe jengo la wodi ya wanaume, Mimi ninatoa mifuko 200 ya saruji kama mchango wa ujenzi wa jingo hilo,” Aliyasema Mkuu wa Mkoa Aprili 17, 2018 alipokuwa anahitimisha ziara ya siku moja katika Halmashauri ya mji Nanyamba.
Aidha katika ziara hiyo Mkuu wa mkoa alitembelea sahemu tofauti kukagua miradi ya maendeleo inayoendelea katika Halmashauri ya mji Nanyamba. Akiwa Nanyamba mkuu wa mkoa alikagua mradi wa ujenzi wa nyumba ya Mkurugenzi, mradi wa ujenzi wa kituo cha Afya cha Dinyecha, ujenzi wa shule ya Sekondari Dinyecha na kutembelea chuo cha maarifa ya nyumbani kinachomilikiwa na shirika la kidini kabla ya kwenda kijiji cha Majengo ambako alihitimisha ziara yake.
Mkuu wa Mkoa Mhe. Gelasius Gaspar Byakanwa akipokea maelezo kutoka kwa Mhandisi alipokuwa anakagua ujenzi wa nyumba ya Mkurugenzi.
NANYAMBA, MTWARA.
Sanduku la Barua: P.O.BOX 1490,
Simu: +255
Simu:
Barua pepe: td@nanyambatc.go.tz
Copyright ©2016 Nanyambatc . All rights reserved.