Kampeni ya Huduma ya Msaada wa Kisheria ya @mslegalaidcampaign ikiwa katika Halmashauri ya Mji Nanyamba tarehe 30 Januari 2025 imeendelea kutoa huduma za Kisheria bure kwa Wananchi mbalimbali Kwa lengo la Kutatua Migogoro mbalimbali inayowakabili ili kuimarisha Ustawi wa Jamii na Usawa katika Taifa.Aidha kwa upande wa mratibu wa Kampeni hiyo ndg @kabado kutoka wizara ya @katibanasheria_ , pamoja na kutoa elimu mbalimbali lakini pia wakapata nafasi ya kukutana na kuzungumza na mwananchi mmoja mmoja kwa kusikiliza changamoto zao zinazowakabili na ili ziweze kutatuliwa kwa haraka.Hata hivyo kwa upande wao baadhi ya wananchi kutoka vijiji vya Arusha Chini, Navikole na Chawi ambao wamefikiwa na huduma hiyo wamemshukuru Mhe.Rais Dokt @samia_suluhu_hassan kwa kuwasogezea huduma hiyo katika ngazi ya chini kabisa ambapo wanaelimishwa na kupewa miongozo mbalimbali ya Kisheria na namna ya kufanya wanapokutana na changamoto zinazohitaji msaada wa kisheria.
NANYAMBA, MTWARA.
Sanduku la Barua: P.O.BOX 1490,
Simu: +255
Simu:
Barua pepe: td@nanyambatc.go.tz
Copyright ©2016 Nanyambatc . All rights reserved.