atika kuhakikisha Wananchi wanapatiwa huduma za kisheria Leo tarehe 27/1/2025 imeendelea na kampeni hiyo ya @mslegalaidcampaign katika kata ya Njengwa.Wananchi wa vijiji vya Malongo, Majengo na Njengwa wamefurahiswa na huduma hiyo ya msaada wa kisheria kwa kujua haki zao zilizokuwa zikiwasumbua kwa muda mrefu.Aidha Wananchi hao walimpongeza Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania kwa ubunifu huo ili Wananchi hao wapate huduma hiyo ya kisheria, kutokana na msaada huo wa kisheria walisema kuwa ingekuwa huduma hiyo toka muda mrefu kwenye ardhi migogoro midogo midogo isiyo na tija ingetatuliwa bila vikwazo vingi
Katika kutoa huduma ya msaada wa kisheria Mji Nanyamba Mratibu wa kampeni hiyo ya Mama Samia Legal Aid Ndg Christopher kabado Kabado aliwaeleza Wananchi wa Kata hiyo kuwa huduma hiyo ni bure na inaratibiwa na wizara ya katiba na Sheria ni kampeni ya nchi nzima yenye lengo la kuwasaidia Wananchi wasioweza kufahamu haki zao za kimsingi kisheria.
NANYAMBA, MTWARA.
Sanduku la Barua: P.O.BOX 1490,
Simu: +255
Simu:
Barua pepe: td@nanyambatc.go.tz
Copyright ©2016 Nanyambatc . All rights reserved.