Wananchi wa kata ya Nyundo katika kuhakikisha wanapatiwa msaada wa kisheria ya @mslegalaidcampaign leo tarehe 29/1/2025 wananchi wa vijiji vya Nyundo, Nyundo B na Niyumba wamepatiwa elimu ya msaada wa kisheria inayotolewa na wataalam mbalimbali ikiongozwa na Ndg @kabado_christopher_ kutoka Wizara ya @katibanasheria ambae ndiyo mratibu wa Kampeni hiyo katika Halmashauri ya Mji Nanyamba.Ndugu Juma Chikota wa kijiji cha Nyundo ameishukuru Serikali ya awamu ya sita kwa kuanzisha programu hiyo inayosimamiwa na wizara ya katiba na Sheria isiwe inatoa elimu hiyo mara moja kwa mwaka kwasabau kwa muda mchache waliotoa elimu hiyo wameipokea kwa mikono yote kwa mfano mambo ya usuluhishi wa migogoro ya ardhi kupitia mabaraza ya kata wametambua hawana mamlaka ya kutoa maamuzi bali wanasuluhisha tuu.Aidha kwa upande wa mratibu wa kampeni Halmashauri ya Mji Nanyamba alisema kuwa kampeni hiyo imeanzishwa mahususi kwa lengo la kuwasaidia Wananchi kujua haki zao za msingi na kutambua wakipatwa na shida ya kisheria waanzie wapi, huduma hiyo haina gharama yoyote kwa Mwanachi atakayehitaji kupata hudmua hiyo ya kisheria alimalizia kwa kusema maneno..
NANYAMBA, MTWARA.
Sanduku la Barua: P.O.BOX 1490,
Simu: +255
Simu:
Barua pepe: td@nanyambatc.go.tz
Copyright ©2016 Nanyambatc . All rights reserved.