Mwalimu Mkuu wa shule ya msingi Namambi, Matiko Hashim Matiko (Mwl) akishirikiana na serikali ya kijiji cha Namambi, kata ya Mnima wameamua kujenga chumba kimoja cha darasa katika shule yao ili kupunguza adha ya wanafunzi wengi kurundikana katika chumba kimoja cha darasa.
Akizungumza na Afisa Habari wa Halmashauri ya Mji Nanyamba, Mwalimu Mkuu huyo amesema, "Tunatekeleza ilani ya chama kwa kuhakikisha tunakata kiu ya muda mrefu kwa wananchi kusimamia na kuhimiza upatikanaji wa maendeleo yenye tija, katika kuharakisha upatikanaji wa elimu bora kwa kuongeza miundombinu madhubuti, tumeamua kujenga chumba kimoja cha darasa kupitia nguvu za wananchi kijiji cha Namambi. Hakika nisiwe mchoyo wa kushukuru hakika timu yangu nikiwa ndie kiongozi nahakikisha tunacheza kwa kupeana pasi na ndio mafanikio ya ushindi kwa kila jambo ambalo tumekuwa tunalibuni."
Aidha, Mwl. Matiko amewasifu na kuwashukuru wananchi wa Kijiji cha Namambi kwa ushirikiano wanaoutoa kufanikisha ujenzi huo unakamilika kwa wakati.
Pia, Mwalimu Mkuu ametoa shukran zake kwa Mkurugenzi wa Mji Nanyamba huku akieleza kuwa amekuwa mtu wa kufikika, kushauri na kusikiliza pale ambapo watumishi wa chini wanapokuwa na shida.
NANYAMBA, MTWARA.
Sanduku la Barua: P.O.BOX 1490,
Simu: +255
Simu:
Barua pepe: td@nanyambatc.go.tz
Copyright ©2016 Nanyambatc . All rights reserved.