Baada ya Mkurugenzi wa Halmashauri ya Mji Nanyamba, Bi. Zainabu S. Mgomi, kutambulisha rasmi utekelezaji wa miradi ya BOOST, wananchi wa vijiji vya Namtumbuka na Niyumba wameonesha moyo wa kizalendo kwa kujitokeza kwa wingi kushiriki kazi za maendeleo.
Wananchi hao wameanza kusafisha maeneo yaliyotengwa kwa ajili ya ujenzi wa miundombinu ya shule, Hatua hii ni ishara ya ushirikiano mzuri kati ya serikali na jamii katika kuhakikisha watoto wanapata mazingira bora ya kujifunzia.
Halmashauri ya Mji Nanyamba inatoa pongezi kwa wananchi wote wanaoshiriki katika kazi hizi na inawahimiza kuendelea kushikamana kwa ajili ya kufanikisha maendeleo endelevu kupitia mradi huu muhimu wa BOOST.
NANYAMBA, MTWARA.
Sanduku la Barua: P.O.BOX 1490,
Simu: +255
Simu:
Barua pepe: td@nanyambatc.go.tz
Copyright ©2016 Nanyambatc . All rights reserved.