Afisa Tarafa ya Nanyamba kwa niaba ya Mkuu wa Wilaya ya Mtwara Mhe Abdallah Mwaipaya leo tarehe 28 Februari 2025 ameshiriki kikao Cha tathimini ya Utekelezaji wa viashiria vya Mkataba wa afua za lishe ngazi ya kata robo ya pili katika ukumbi mdogo wa Halmashauri ya Mji Nanyamba.Akizungumza kwa kwa niaba ya Mkuu wa Wilaya Afisa Tarafa ya Nanyamba Ndg Seif Nanyembe awasihi watendaji hao wa Kata kuendelea kusimamia vizuri viashiria vya mkataba wa afua za lishe ngazi ya kata kama maelekezo ya Serikali kupitia Wizara ya @or tamisemi ilivyoelekeza.Afisa lishe wa Mji Nanyamba Bi Pilly Mpelenganj akitoa taarifa ya tathimini ya utekelezaji wa viashiria vya Mkataba wa afua za lishe ngazi ya kata alisema kuwa kwa robo ya pili mwaka wa fedha 2024/2025 Halmashauri imetekeleza kwa asilimia 96.1%.
NANYAMBA, MTWARA.
Sanduku la Barua: P.O.BOX 1490,
Simu: +255
Simu:
Barua pepe: td@nanyambatc.go.tz
Copyright ©2016 Nanyambatc . All rights reserved.