Waziri wa kilimo Mhe @bashehussein ametoa maelekezo kwa Mkurugenzi wa Bodi ya korosho ifikapo msimu wa korosho mwaka 2025 katika eneo hilo la kongani ya viwanda lianze kufanya kazi kwa kujenga kiwanda cha ubanguaji wa korosho.
Waziri Bashe alisema kuwa kiwanda hicho angalau kiwe cha kubangua Tani 3000 kwa siku uwezo huo upo na kazi hiyo ifanyike ili wananchi wa Maranje waanze kupata keki ya Taifa kupitia mradi huu amesema leo tarehe 1 Octoba 2024 baada ya kukagua eneo la ujenzi unaoendelea wa maghala mawili yatakayobeba korosho kila ghala moja tani 10000.
NANYAMBA, MTWARA.
Sanduku la Barua: P.O.BOX 1490,
Simu: +255
Simu:
Barua pepe: td@nanyambatc.go.tz
Copyright ©2016 Nanyambatc . All rights reserved.