Ziara ya siku tatu ya Waziri Mkuu wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mhe. Majaliwa Kassim Majialiwa iliyokamilika February 28, 2018 ilikuwa na mengi ambayo yanaacha alama ya jitihadakubwa ya Mkoa wa Mtwara katika kutafasiri falsafa ya HAPA KAZI TU.
Ziara hiyo ambayo imehitimishwa kwa kufanya mkutano na wananchi wa Mji wa Nanyamba, wilaya ya Mtwara. Waziri Mkuu amewaeleza wananchi juu ya msimamo wa serikali ya awamu ya tano kuwa serikali imedhamiria kuwahudumia wananchi, kusimamia nidhamu na kuwawajibisha watumishi wazembe huku akisisitiza kuwa wala rushwa kutokuwa na nafasi katika serikali ya awamu hii ya tano.
Aidha, Waziri Mkuu aliwaambia wananchi wa Nanyamba, pamoja ma jitihada ambazo serikali inazifanya katika sekta ya elimu bado hali ya elimu kwa Nanyamba na Mkoa wa Mtwara kiujumla si mzuri huku akisisitiza wananchi kusimamia mienendo ya masomo ya watoto wao. Waziri Mkuu aliedelea kuwataka wazazi wa wahudumie watoto wao kwa kuwanunulia sare za shule, kuwalisha vizuri na kuhakikisha wanaenda shuleni.
Mhe. Waziri Mkuu amesema, “Serikali imeendelea kuhimarisha sekta ya elimu kwani tayari tumeshaleta pesa za ukarabati kwa shule za msingi na sekondari lakini pia tunaleta vifaa kwa ajili ya maabara hivyo ni jukumu la Mkurugeenzi kumaliza ujenzi wa hizo maabara”. Katika hili, Waziri Mkuu ameeleza kuwa serikali imeleta million 130 kwa ajili ya ujenzi wa madarasa 6 na vyoo 12 katika shule za Msingi za Mikumbi na Chiwilo, na milioni 712 kwa shule za sekondari.
Katika hotuba yake, Mhe. Waziri Mkuu amewataka vijana wanaowalaghai wanafunzi wa kike na kushirikiana nao kimahusiano kuacha tabia hiyo mara moja kwani serikali imedhamiria kuweka sharia ngumu dhidi ya watu hao huku akisistiza kwa wanaNanyamba kuhakikisha watambue kuwa wao wote ni wazazi wa vijana hao hivyo hawana budi kuhakikisha vijana wanamaliza masomo yao bila kukatishwa.
Kuhusu nishati ya Umeme, Waziri Mkuu amesema ni kweli kuna tatizo la umeme kwa mikoa ya Lindi na Mtwara. Ameeleza chanzo cha tatizo hilo ni kuharibira kwa mashine 7 kati ya 9 zilizopo katika chanzo cha kuzalisha umeme huo. Waziri Mkuu amesema tayari mashine 5 kati ya 7 zimekarabatiwa na mbili zimenunuliwa hivyo kilichobakia ni kuunganisha tayari kwa uzalishaji wa umeme.
Aidha, Waziri Mkuu alisema, “Hili jambo la umeme ili kuliweka sawa tumeamua mikoa ya Lindi na Mtwara tuiunganishe na gridi ya taifa kwa maana umeme utatoka Dar es Salaam na tayari Serikali imeshajenga kituo cha kupokelea umeme pale Maumbika, Mnazi mmoja. Na kama vile haitoshi, Serikali inajenga laini nyingine ya kutoka Makambako kupitia Njombe, Songea, Namtumbo, Tunduru na kuunganisha Masasi na kuingia Lindi na Mtwara.”
Kuhusu Korosho, Waziri Mkuu amemsifu Mkuu wa Mkoa wa Mtwara pamoja na Mkuu wa Wilaya kwa jitihada na hatua walizozichukua dhidi ya viongozi wa vyama vya msingi vitatu; Kilimanjaro, Mnongodi na Mkombozi AMCOSS kwa kuwakeka ndani na kuwataka warejeshe pesa za wakulima. Waziri Mkuu amewataka viongozi wa vyama vya msingi kuacha tabia ya kuiba pesa za wakulima huku akisisitiza ya kuwa endapo kuna kiongozi amewaza kujitajirisha kupitia vyama hivyo basi ni vema akijiuzuru kabla serikali haijamfikia kwani Serikali ya awamu ya tano imejipambanua kudili na watu kama hao katika kutetea maslahi ya wakulima.
“Nanyamba, Tandahimba, Newala zote ni wilaya zote; Korosho ni uchumi wa mtu mmoja mmoja, mtu yeyote atakayetaka kuingilia kati na kusababisha uchumi usipatikane Serikali itakufa nae”, alisema Waziri Mkuu.
NANYAMBA, MTWARA.
Sanduku la Barua: P.O.BOX 1490,
Simu: +255
Simu:
Barua pepe: td@nanyambatc.go.tz
Copyright ©2016 Nanyambatc . All rights reserved.