Mhe. Kassim Majaliwa Waziri Mkuu wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania (Mb) leo Tarehe 08.07.2023 amefanya ziara ya kikazi Halmashauri ya Mji Nanyamba.
Katika Ziara hiyo ametembelea Jengo la Utawala la Halmashauri ya Mji Nanyamba, ametembelea na kukagua mradi wa ujenzi wa mabweni, Vyumba vya madarasa, na matundu ya vyoo vyenye thamani ya Bilioni 1.2 Shule ya sekondari Dinyecha unaofadhiriwa na kampuni ya Barrick Gold Mine pamoja na Fedha kutoka Serikali Kuu na kufurahishwa na utekelezaji unavyoendelea.
Pia Mhe. Kassim Majaliwa amezungumza na wananchi wa Halmashauri ya Mji Nanyamba katika viwanja vya Shule ya Msingi Nanyamba Ufundi huku akiwasisitiza Watumishi kuwatumikia wananchi katika kutatua changamoto zao. Pia katika Hotuba yake alitoa maelezo kuwa pesa zinazotolewa kwenye Sekta ya Afya zitumike kama zilivyopangiwa na wananchi wapate Dawa hizo bila kubuguziwa kwa kuwataka wakanunue maduka ya Dawa.
Nae, Mbunge wa Jimbo la Nanyamba Mhe. Abdallah Dadi Chikota ameishukuru Serikali ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania kwa kuiona Nanyamba kwa kuleta Fedha za Miradi mbalimbali ya kimkakati na ile isiyoya kimkakati.
NANYAMBA, MTWARA.
Sanduku la Barua: P.O.BOX 1490,
Simu: +255
Simu:
Barua pepe: td@nanyambatc.go.tz
Copyright ©2016 Nanyambatc . All rights reserved.