Waziri wa kilimo Mhe @bashehussein akiongea na wananchi wa Halmashauri ya Mji Nanyamba katika kijiji cha Maranje Kata ya Mtiniko leo tarehe 1/10/2024 amesema kuwa malipo ya korosho msimu wa mwaka 2024 yatalipwa moja kwa moja na Vyama Vikuu vya ushirika na si tena Vyama vya Msingi yaani AMCOS kuondoa ubabaishaji uliokuwa ukifanywa na vyama vya Msingi.
Hayo yamesemwa mbele ya wananchi hao mara baada ya kutembelea na kuona eneo la kongani ya viwanda lililoanza kutekelezwa kujengwa kwa kuanza na maghala mawili ya tani 10000 kila moja.
Waziri bashe aliendelea kusema hadi kufika mwaka 2027 eneo hilo liwe lishakamilika ila kwa kuanza msimu wa mwaka 2025 kiwanda cha ubanguaji wa korosho cha tani 3000 kiwe kimeshakamilika aliongeza kwa kusema kuwa fedha zipo hadi mwaka huo zaidi ya bilioni 300 zinahitaji kukamilisha mradi huo.
Mheshimiwa Bashe ameiagiza Bodi ya korosho kuwa bega kwa bega na mkandarasi ili mradi huo ukamilike kwa wakati kiasi cha Shilingi Bilioni 7 zimeshaletwa kwaajili ya ujenzi wa kongani huku serikali ikiendelea kutafuta wawekezaji wengine.
Kusudio la mradi huo wa kongani ni mahsusi kwa serikali korosho ghafi zibanguliwe haoa hapa nchini zote na ziweze kusafirishwa nchi mbalimbali korosho zilizopekiwa kwaajili ya kuliwa alisema waziri Bashe.
Mwisho aliwapongeza wananchi wa vijiji vya maranje na Tulia kata ya Mtiniko kwa kukubali kutoa maeneo yao kwa kufuta jasho na si fidia malipo yake watayaona vizazi vijavyo alimalizia kwa kusema maneno hayo
NANYAMBA, MTWARA.
Sanduku la Barua: P.O.BOX 1490,
Simu: +255
Simu:
Barua pepe: td@nanyambatc.go.tz
Copyright ©2016 Nanyambatc . All rights reserved.