Leo tarehe 30/1/2025 Taasisi isiyo ya Kiserikali ijulikanayo Kongwa Trachoma Project (KTP) Makao Makuu yake Kongwa Jijini Dodoma imezindua huduma ya usawazishaji wa Vikope katika kata ya Nyundo.
Mkurugenzi wa Kongwa Trachoma Project (KTP) Ndg Harran Mkocha amesema kuwa huduma kwa Mkoa wa Mtwara Halmashauri zilizonufaika na mradi huo ni Halmashauri ya Wilaya Nanyumbu, Halmashauri ya Mji Masasi, Halmashauri ya Mji Newala pamoja na Halmashauri ya Mji Nanyamba.Mkurugenzi huyi alisema kuwa kwa Mji Nanyamba Kata zote 17, vijiji na Mitaa itapitiwa na huduma hiyo nyumba hadi nyumba ni mradi utakaodumu zaidi ya mwaka mmoja na miezi nane zaidi ya Wananchi 800 wataoatiwa huduma hiyo ya usawazishaji wa vikope.Dkt Otilia Flavian Gowelle kwaniaba ya Mkurugenzi wa Idara ya Kinga kutoka @wizara_afyatz ameishukuru Taasisi ya Kongwa Trachoma Project kwa kutambua kutoa huduma kwenye magonjwa yaliyokuwa hayapewi kipaumbele kama vile Ugonjwa wa Trachoma, Dkt Otilia aliwahakikishia Taasisi hiyo kama wizara ya afya kuunga nao muda wote wanapohitaji msaada toka wizarani.Kwa upande wa Mganga Mkuu wa Mkoa wa Mtwara Dkt Benedicto Ngaiza aliwashukuru Kongwa Trachoma Project kwa kuja Mkoa wa Mtwara ili wasaidie wananchi wa mkoa huo alisisitiza kuwa kupitia Waganga wa Halmashauri husika watatoa ushirikiano muda wote ili huduma zitolewazo wananchi wanufaike kwasababu huduma hiyo ya usawazishaji wa Vikope ni bure hakuna gharama mwananchi anayochangia.
NANYAMBA, MTWARA.
Sanduku la Barua: P.O.BOX 1490,
Simu: +255
Simu:
Barua pepe: td@nanyambatc.go.tz
Copyright ©2016 Nanyambatc . All rights reserved.