Halmashauri ya Mji Nanyamba imefanya ziara Maalumu ya utambuaji wa Maafisa Usafirishaji(bodaboda) waliopo Halmashauri ya Mji Nanyamba vituo vyake katika kata zote zilizopo Halmashauri kwa lengo la kuwatambua na kurahisisha utoaji wa huduma za kiusalama kwao mnamo tarehe 11/12/2024.
Pia zoezi hilo liliambatana na utoaji wa elimu ya Barabarani kwa maafisa hao wasafirishaji yaani bodaboda ili kuweza kuwajengea uwezo wa kutambua sheria muhimu za barabarani ili waweze kufuata sheria hizo za barabarani.Zoezi hilo limeratibiwa na Ndugu Nassoro Jamala Mnyika Afisa mipango kutoka Halmashauri Ndugu Magai Kamanda wa polisi usalama barabarani Mji Nanyamba, Ndugu Dini Litimba Mwenyekiti wa Bodaboda Halmashauri Pamoja na Ndugu Salumu Chawaka katibu wa Bodaboda Halmashauri.
NANYAMBA, MTWARA.
Sanduku la Barua: P.O.BOX 1490,
Simu: +255
Simu:
Barua pepe: td@nanyambatc.go.tz
Copyright ©2016 Nanyambatc . All rights reserved.