Mapato ya Nanyamba na Msimu wa korosho.
Msimu wa korosho ndio kipindi pekee cha pilika nyingi
za kiuchumi na kijamii kwa wakazi wa mji wa Nanyamba,
mambo yote haya hufanyika ndani ya miezi minne,
miezi miwili ya mwaka husuka na miezi miwili ya mwaka mpya.
Halmashauri hupata ushuru kupitia vyama vya msingi pindi wanapouza korosho
Shuru na tozo mbalimbali zinazolipwa na wakazi wa mji Nanyamba
kwa shughuli mbali za kibiashara na kijamii pia kiutamaduni,
lakini Halmashauri inatumia nguvu nyingi kukusanya mapato kwa kuwalazimisha wahusika kulipa ushuru na tozo
mbalimbali.
Jamii ya Mji wa Nanyamba imekuwa haitambui umuhimu wa kulipa na kodi
na kujihusisha na utoroshaji wa mapato kwa kutoa nje ya vijiji,kata na hata wilaya
pasipo kuumia kuwa wanapoteza mapato ya halmsahuri yao.
kupitia makala hii fupi halmsahuri inawaomba wananchi wote wa mji Nnaymba kuelewa kuwa
ulipaji wa kodi mbalimbali ni muhimu kwa ustawi wa Nanyamba na Taifa kwa ujumla.
wananchi wasijihusishe kutorosha mapato ya Halmasshauri na watambue nikosa kufanya hivyo.
pamoja na Halmashauri kuwakamata wahusika bado baadhi ya watu wameendelea kufanya
kosa hilo kwa makusudi.
Halmasahuri inaendelea na operation ya kukusimamia,kukusanya na kuibua vyanzo vipya vya mapato ili
kuinua kimapato halmaasahuri ya Nanyamba, na jamii isiowaone wahusika ni wabaya
isipo kuwa wawasaidie kwa kulipa kodi bila shuruti.
NANYAMBA, MTWARA.
Sanduku la Barua: P.O.BOX 1490,
Simu: +255
Simu:
Barua pepe: td@nanyambatc.go.tz
Copyright ©2016 Nanyambatc . All rights reserved.