Kaimu mkurugenzi wa halmashuri ya mji Nanyamba Ndugu Hamisi Amani na Mkuu wa idara ya kilimo na mifugo Ndugu
Elias Peter Matoja wamekabidhi kuku jumla ya 600 kwa vijiji vya Nitekela, Nyundo na Njengwa.
kati ya hao 300(kroiler) na 300(sasso) kila kijiji walipatiwa wafugaji 10 na kila mnufaika wa mradi alipatiwa kuku 20.
Mradi huu umefadhiliwa na Serikali ya Jamhuri ya muungano wa Tanzania kupitia wizara ya kilimo na mifugo kitengo
cha maabara, dhamira ya mradi ni kuongeza kipato katika kaya.
Utekelezaji wa mradi huu unatokana na utekelezaji wa ilani ya chama cha mapinduzi chini ya usimamizi wa Rais wa
Jamhuri ya muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Joseph Magufuri ya kuboresha maisha ya wananchi hususani wa vijijin kupitia
miradi mbalimbali.
Wanufaika kwa upande wao wameishukuru serikali kwa kuwakumbuka na kuahidi kuuendeleza mradi huo ili uweze kuleta tija.
NANYAMBA, MTWARA.
Sanduku la Barua: P.O.BOX 1490,
Simu: +255
Simu:
Barua pepe: td@nanyambatc.go.tz
Copyright ©2016 Nanyambatc . All rights reserved.