HAFLA YA UZINDUZI WA MRADI WA UJENZI WA MADARASA KWA FEDHA ZA UVIKO19
Mkuu wa wilaya ya Mtwara Mh Dunstan Kyobya amezindua mradi wa ujenzi wa madarasa 31 wenye
thamani ya Tsh 620000000/= (mia sita ishirini milioni) kutokana na fedha za UVIKO19 zilizotolewa na Mh Rais wa Jamhuri
ya Muungano wa Tanzania Samia Suluhu Hassani uliofanyika viwanja vya shule ya sekondari Nanyamba
Akizungumza katika hafla hiyo Mh Dunstan Kyobya amemshukuru Mh Rais kwa niaba ya wananchi
wa Halmashauri ya Mji Nanyamba kwa kuwapatia fedha hizo ambazo zitamaliza kabisa tatizo la madarasa
na madawati pia amewaasa wazazi na jamii kwa ujumla kujitolea katika shughuli mbalimbali wakati wa utekelezaji
wa mradi huo ili kuhakikisha mradi unakamilka kwa wakati
Katika uzinduzi huo Mkurugenzi wa Halmashauri ya Mji Nanyamba Ndugu Thomas Edwin Mwailafu amemshukuru Mh Rais
wa Jamhuri ya muungano wa Tanzania kwa fedha hizo na ameahidi kuzisimamia kwa menejimenti yake ili kuhakikisha
mradi unatekelezwa kwa wakati na kwa uadilifu ili uwe wenye tija na kuwaagiza wazazi na walezi wote kuwapeleka shule
wanafunzi wote waliohitimu darasa la saba na kuchaguliwa kujiuunga na kidato cha kwanza kwa mwaka wa masomo 2021/2022
Kwa upande wake mwenyekiti wa Halmashauri ya Mji Nanyamba Mh Jamar Abdallah Kapende amewaasa waheshimiwa
madiwani na wananchi ambao watateuliwa kuwa katika kamati za ujenzi kuwa waadilifu na kutanguliza uzalendo katika utekelezaji
wa mradi huu kwani hakuna pesa ambayo itatengwa kwa ajiri ya posho na kutoa angalizo kuwa kama yuko mtu anahisi atajipatia fedha
kwa maslahi binafsi ni bora akajiondoa mapema kwani hizi fedha ni za moto na zitatumika tu vile ilivyokusudiwa na si vinginevyo
Mradi huu unatekelezwa katika shule zote 11 za sekondari katika Halmashuri ya Mji Nanyamba kwa mchanganuo ufuatao
NAMBA | JINA LA KATA | JINA LA SHULE | IDADI YA MADARASA | FEDHA KWA DARASA MOJA | JUMLA |
1 | NJENGWA | NJENGWA SS | 3 | 20,000,000/= | 60,000,000/= |
2 | NANYAMBA | NANYAMBA SS | 3 | 20,000,000/= | 60,000,000/= |
3 | CHAWI | CHAWI SS | 2 | 20,000,000/= | 40,000,000/= |
4 | DINYECHA | DINYECHA SS | 2 | 20,000,000/= | 40,000,000/= |
5 | KIROMBA | KIROMBA SS | 3 | 20,000,000/= | 60,000,000/= |
6 | KITAYA | KITAYA SS | 2 | 20,000,000/= | 40,000,000/= |
7 | MBEMBALEO | MBEMBALEO SS | 2 | 20,000,000/= | 40,000,000/= |
8 | MILANGOMINNE | MNYAWI | 3 | 20,000,000/= | 60,000,000/= |
9 | MTIMBWILIMBWI | MTINIKO SS | 3 | 20,000,000/= | 60,000,000/= |
10 | NITEKELA | NITEKELA SS | 3 | 20,000,000/= | 60,000,000/= |
11 | MNIMA | MNIMA SS | 2 | 20,000,000/= | 40,000,000/= |
12 | NYUNDO | NYUNDO SS | 3 | 20,000,000/= | 60,000,000/= |
JUMLA |
|
|
31 | @ 20,000,000/ | 620,000,000/= |
NANYAMBA, MTWARA.
Sanduku la Barua: P.O.BOX 1490,
Simu: +255
Simu:
Barua pepe: td@nanyambatc.go.tz
Copyright ©2016 Nanyambatc . All rights reserved.